Baraza la Usalama la UN laongeza vikwazo vya silaha Haiti
19 Oktoba 2024Wanachama wote 15 wa Baraza hilo la Umoja wa Mataifa walipigia kura azimio hilo, ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzuia usafirishaji wa silaha za aina yoyote kuingizwa Haiti.
Vikwazo vilivyowekwa awali, vililenga tu silaha ndogo ndogo na risasi.
Azimio liliwasilishwa na Ecuador na Marekani
Azimio hilo lililowasilishwa jana na Ecuador na Marekani, pia linajumuisha kuongezwa muda wa mwaka mmoja kwa kamati ya kufuatilia vikwazo dhidi ya baadhi ya raia wa Haiti.
Mwakilishi wa Marekani, Dorothy Shea, aliliambia Baraza hilo kwamba hali nchini Haitibado ni mbaya mno.
Shea ameongeza kuwa Marekani bado ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu nchini Haiti na kwamba watu wengi bado wanaendelea kuteseka kutokana na vurugu hizo zinazoendelea.