1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Baraza la UN lataka kusitishwa zaidi kwa vita Gaza

16 Novemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito wa kurefushwa kwa usitishaji mapigano chini ya misingi ya kiutu kwenye mzozo wa Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4Yr90
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano kuhusu mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas katika makao makuu ya Umopja huo mjini New York nchini Marekani Oktoba 25, 2023
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano kuhusu mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la HamasPicha: David Dee Delgado/REUTERS

Hiyo ni mara ya kwanza kwa baraza hilo lenye jukumu la kusimamia amani ya ulimwengu kuvunja ukimya tangu kuanza kwa mzozo mbaya kabisa kati ya Israel na kundi la Hamas. Kwenye kikao cha Jumatano jioni, baraza hilo limepitisha azimio lililoandaliwa na Malta na kupata uungaji mkono wa wanachama 12 wengine.

Azimio lataka kuheshimiwa kwa sheria ya kuwalinda raia hasa watoto

Marekani, Uingereza na Urusi zilijizuia kulipigia kura azimio hilo lililofikishwa mbele ya baraza la usalama lenye nchi 15 wanachama. Karibu kila aya ya azimio hilo limewataja watoto hususani likitaka "pande zote kuheshimu sheria ya kimataifa kuwalinda raia, hasa hasa watoto".