1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bavaria yazuia mashabiki uwanjani mechi za Bundesliga

Sylvia Mwehozi
3 Desemba 2021

Mechi za mpira wa miguu Ujerumani katika jimbo la Bavaria zitachezwa bila ya mashabiki uwanjani kwa hivi sasa kutokana na wimbi la nne la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/43neG
Fußball Bundesliga | Hertha - Augsburg
Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Mechi za mpira wa miguu Ujerumani katika jimbo la Bavaria zitachezwa bila ya mashabiki uwanjani kwa hivi sasa kutokana na wimbi la nne la virusi vya corona.

Waziri Mkuu wa jimbo la Bavaria Markus Soeder amesema uamuzi huo unaanza kutumika Jumamosi (04.12.2021) na utaathiri michezo yote na ligi za kikanda.

Mechi za nyumbani za Bundesliga kati ya Augsburg dhidi ya Bochum na ile ya daraja la pili baina ya Nurenmberg na Holstein Kiel zitachezwa bila ya mashabiki uwanjani siku ya Jumamosi.

Mabingwa wa Bundesliga na vinara wa ligi Bayern Munich wanasafiri kuwakabili mahasimu wao Borussia Dortmund siku ya Jumamosi.

Serikali ya shirikisho na viongozi wa majimbo wamekubaliana kiasi cha mashabiki 15,000 au asilimia 50 ya uwezo wa uwanja ambao wataruhusiwa katika mchezo huo ikiwa jimbo halitoondoa kanuni za sasa.

Katika jimbo la Saxony ambako ndipo ilipo timu ya RB Leipzig tayari imetangazwa mechi bila ya mashabiki. Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema hatua ya kuwaruhusu mashabiki 15,000 ni lazima itekelezwe kikamilifu. Hiyo ni pamoja na kuwaruhusu wale tu waliochanjwa au waliopima na uvaaji wa barakoa.