1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaanza vyema mbio za Champions. Yaichakaza Zagreb 9-2

18 Septemba 2024

Mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani Harry Kane amefunga magoli manne na kuiongoza timu yake kuicharaza timu ya Dinamo Zagreb mabao 9-2 siku ya Jumanne

https://p.dw.com/p/4kjrF
Champions League |  Bayern München
Harry Kane, ameifungia timu yake ya Bayern Munich mabao 4 kati ya 8 dhidi ya Dinamo Zagreb, katika michuano ya Champions, Septemba 18, 2024Picha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Bayern Munich imeweka rekodi ya magoli mengi yaliyofungwa na timu moja kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kane alifunga mabao matatu kwa mikwaju ya penati, na kuanzisha vyema mbio za ubingwa wa Champions za kikosi hicho kinachoongozwa na Vincent Kompany, ambacho hakikushinda kombe lolote la ndani ama kimataifa msimu uliopita.

Mechi nyingine zilizowahi kuvunja rekodi ya magoli mengi ni kati ya Liverpool na Real Madrid iliyoshuhudia mabao 8-0 na Borussia Dortmund iliyoifunga Legia Warsaw, mabao 8-4

Kylian Mbappé naye amerejesha matumaini yake ya kushinda kombe hilo bada ya kuisaidia timu yake ya Real Madrid ya Uhispania kuondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stutgart ya Ujerumani, katika uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.