1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yatekwa, Dortmund yashika kasi

1 Septemba 2014

Mmoja wa wachezaji wapya katika Bundesliga ni kiungo Xabi Alonso ambaye hakumaliza hata saa 24 baada ya kujiunga na Bayern, na akacheza mechi yake ya kwanza waliyotoka sare ya goli moja kwa moja na Schalke.

https://p.dw.com/p/1D4tO
Fußball Bundesliga FC Schalke 04 vs. FC Bayern München Alonso
Picha: Getty Images

Alonso ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Bayern kutoka Real Madrid alikuwa na pasi nyingi zaidi uwanjani kuwaliko wachezaji wake. Mhispania huyo anakiri kuwa mambo yalimwendea kwa kasi lakini anafurajia kujiunga na ligi ya Soka ya Ujerumani.

"ni hisia tofauti, lakini nilijihisi vyema kwa sababu kuwa sehemu ya klabu kubwa kama Bayern Munich kwa kawaida ni kitu cha kujivunia na cha heshima kubwa. Na nina uhakika, kuwa nitakavyoizoea timu hii, wenzangu watanifahamu vyema, name nitawaelewa. Nitazungumza na mkufunzi kuhusu kile anachotaka nikifanye, kwa hivyo ntahitaji muda kidogo".

Wakati huo huo, Bayer Leverkusen walijifunga goli katika lango lao na kisha wakatoka nyuma mara mbili na kuwazaba Hertha Berlin magoli manne kwa mawili, ili kuendelea kusalia kileleni mwa Bundesliga, baada ya kushinda mechi mbili kati ya mbili za mwanzo wa msimu.

Borussia Dortmund waliponea kishindo cha kipindi cha pili kutoka kwa Augsburg, na wakashinda magoli matatu kwa mawili. Habari nzuri kwa BvB zilikuwa kurejea kwa Marco Reus ambaye alikuwa nje ya Kombe la Dunia kutokana na jeraha, lakini sasa amerudi kwa kishindo.

Katika matokeo mengine ya mechi zilizochwezwa jana, Borussia Moenchengladbach walitoka sare ya kutofungana goli na Freiburg, wakati Hanover 96 wakipata matokeo hayo hayo dhidi ya Mainz.

Mwandishi; Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Saumu