Bei ya unga huko Kenya huenda ikapanda baada ya serikali kuwaruhusu wafanyabiashara wa kusaga mahindi kuagiza magunia milioni 4 kutoka nchini Mexico. Shehena ya kwanza ya mahindi hayo inatarajiwa kuwasili mwezi wa Julai mwaka huu. Duru zinaeleza kuwa mahindi yaliyoko kwenye ghala la taifa yameoza na yana sumu ya aflatoxin. Msikilize Thelma Mwadzaya.