Benki ya Dunia na IMF zaanza mkutano ya juma zima
10 Aprili 2023Matangazo
Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Ulimwenguni, IMF, zitaendelea na mikutano yake juma hili kwa nia ya mageuzi huku kukiwa na matarajio ya kugubikwa na ajenda kabambe za mashaka ya mfumko wa bei na kuongezeka kwa mivutano na umadhubuti wa hali ya kifedha kote duniani.
Katika hotuba yake ya juma lililopita, Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva, amenukuliwa akisema "Ukuaji wa uchumi unasalia kuwa dhaifu, kwa sasa na katika muda wa kati."
Mfuko huo kwa sasa unatarajia ukuaji wa uchumi kimataifa kupungua chini ya asilimia tatu mwaka huu, na kubaki karibu na asilimia tatu kwa nusu muongo ujao ikiwa ni kiwango cha chini kabisa cha utabiri wa muda wa kati tangu katika miaka ya 1990.