1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUfaransa

Benki ya Dunia yazindua mkakati kusaidia nchi zenye majanga

22 Juni 2023

Benki ya Dunia imetangaza msururu wa hatua za kuyasaidia mataifa yaliyoathiriwa na majanga ya asili, ikiwa ni pamoja na kusimamisha malipo ya madeni kwa wakopeshaji.

https://p.dw.com/p/4Swzl
Frankreich Gipfel des neuen globalen Finanzpakts in Paris
Picha: Ludovic Marin/REUTERS

Imetangaza hatua hizo katika mkutano wa kilele wa viongozi wa ulimwengu wanaokutana mjini Paris unaolenga kutoa msukumo wa ajenda ya kifedha katika mapambano ya mabadiliko ya tabianchi.

Soma pia: Macron afungua mkutano wa kilele wa ufadhili wa fedha za hali ya hewa

Kwenye hotuba yake mapema leo, rais wa Benki hiyo Ajay Banga ameainisha mpango huo utakaojumuisha pia na kuziwezesha nchi kupeleka fedha maeneo mengine kushughulikia dharura, kuanzisha aina mpya za bima zitakazosaidia miradi ya maendeleo na kuzisaidia serikali kujenga mifumo ya kisasa zaidi ya kukabiliana na dharura. "Rais wa Benki ya Dunia: Na muhimu zaidi ni kusitisha ulipaji wa madeni ili mataifa yaweze kuzingatia kile ambacho ni muhimu kwa viongozi wakati wanaokumbwa na mzozo badala ya kuhofia deni yatakayokuja baada ya mzozo huo."

Mkakati huo, aidha unalenga kuongeza ufadhili kwa mataifa ya kipato cha chini, kurekebisha mifumo ya kifedha ya baada ya vita na kutoa fedha za kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi.