1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Uganda yasubiri ripoti kuhusu wizi wa dola mil. 17

29 Novemba 2024

Benki ya Uganda imesema inasubiri uchunguzi wa polisi kuhusu taarifa ya vyombo vya habari kwamba wadukuzi wa kigeni wameiba dola milioni 16.8 kutoka kwa benki kuu ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4nYmL
Mashambulizi ya mtandao
Mashambulizi ya mtandaoPicha: Imago/Science Photo Library

Benki ya Uganda imesema inasubiri uchunguzi wa polisi kuhusu taarifa ya vyombo vya habari kwamba wadukuzi wa kigeni wameiba dola milioni 16.8 kutoka kwa benki kuu ya nchi hiyo.

Gazeti la serikali la nchi hiyo la New Vision liliripoti jana kwamba mapema mwezi huu na kuhamisha fedha hizo kwa njia isiyo halali .

New Vision imeripoti kuwa kundi hilo la wadukuzi lililoko Kusini-mashariki mwa Asia, lilituma sehemu ya pesa zilizoibwa nchini Japan,  ikinukuu vyanzo vya benki hiyo ambavyo havikutambulishwa.Askari wanawake Afrika kujadili namna kukabiliana na uhalifu

Kwa kujibu swali la Reuters kupitia barua pepe, Benki hiyo ya Uganda haikuthibitisha wala kukanusha tukio hilo lakini ikasema inasubiri ripoti hiyo ya polisi.

Hata hivyo polisi haikujibu mara moja ombi la tamko kutoka kwa Reuters kuhusu suala hilo.