1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Schroeder aenda mbio kutetea katiba mpya ya Ulaya

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7C

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani,anachukua nafasi ya mbele katika juhudi za kutafuta suluhisho kwa mzozo wa kisiasa kuhusu katiba ya Ulaya.Hii leo mjini Berlin,anakutana na rais Jacques Chirac wa Ufaransa kuujadili mkataba uliokataliwa wiki hii na wapiga kura nchini Ufaransa na Uholanzi.Mkutano wake na Chirac ni mmoja kati ya mlolongo wa mikutano inayofanywa na Kansela Schroeder kutafuta njia za kuyajumuisha madola ya Ulaya,licha ya matukio hayo ya kukatisha tamaa.Ujerumani ni miongoni mwa nchi 10 zilizoidhinisha katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.Lakini wananchi wake hawakupewa nafasi ya kupiga kura ya maoni kuhusu katiba hiyo.