1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mizozo ya Afrika imesahauliwa asema waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Kerstin Muller.

23 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFbY

Waziri wa nchi anayeshughulikia mambo ya nje Bi Kerstin Muller ametahadharisha juu ya kusahauliwa kwa mizozo ya Afrika kutokana na kampeini ya kuzisaidia sehemu za dunia kutokana na maafa ya Tsunami.

Bi Muller amesema hayo mjini Berlin na kuongeza kwamba katika kuzisaidia sehemu nyingine kukabiliana na majanga ya asili Afrika pamoja na nchi Zinazoendelea zisisahauliwe. Waziri huyo Wa Ujerumani hasa amekumbusha juu ya mgogoro wa jimbo la Darfur na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na katika maziwa makuu.