1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Schroeder akabiliwa na pigo la kushindwa katika uchaguzi wa jimbo

22 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBS

Chama cha Social Demokrat cha Kansela Gerhrad Schroeder wa Ujerumani kinakabiliwa na kishindo cha kushindwa leo hii katika uchaguzi wa jimbo la North Rhine- Westphalia ambao yumkini ukawa ndio kigezo kwa uchaguzi mkuu ujao hapo mwakani.

Chama cha SPD kimekuwa kikilitawala jimbo hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Ujerumani kwa karibu miaka 40 lakini uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni umeonyesha kuwa kiko nyuma ya chama cha mrengo wa kulia wa wastani cha Christian Demokrat CDU kwa pointi saba.

Wajerumani milioni 13 wana haki ya kupiga kura katika jimbo hilo la Ujerumani ya magharibi lililokuwa kitovu cha viwanda likiwa na viwanda vingi vya makaa ya mawe na chuma.Masuala ya kitaifa yamehodhi uchaguzi huo hususan kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini Ujerumani.

Kiwango cha ukosefu wa ajira mwaka huu kimefikia milioni tano nchini kote na kupindukia milioni moja kwenye jimbo hilo kutokana kwa kiasi fulani na mageuzi yaliozusha utata ya Schroeder kwa soko la ajira yaliosanifiwa kuchochea uchumi.