BERLIN: Schroeder akaribisha mazungumzo ya Marekani na Ulaya
20 Februari 2005Kansela Gerhrad Schroeder wa Ujerumani ameikaribisha kauli iliyotolewa na Rais George W Bush wa Marekani ya kutaka kuwepo kwa mazungumzo ya kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Ulaya.
Bush na Schroeder wanatarajiwa kuwa na mazungumzo mjini Mainz nchini Ujerumani hapo Jumaatano.Mapema Bush amesema atakukaribisha kushiriki zaidi kwa Ujerumani katika kuijenga upya Iraq.Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Ujerumani cha ARD Bush amesema kwamba msaada wa Ujerumani utathaminiwa sana katika kulijena upya taifa la Iraq na kutowa misaada ya kibinaadamu kama vile inavyofanya nchini Afghanistan.
Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo ya Rais Bush Barani Ulaya ambayo inaanza rasmi leo hii miji kama vile wa Brussels nchini Ubelgiji imekuwa ikichukuwa tahadhari kwa kuimarisha usalama.