1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Schroeder akatiza zaira yake ya kwenda Marekani.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAD

Kansela wa Ujerumani, Gerhard Schroeder, ataifutilia mbali ziara yake rasmi nchini Marekani iliyokuwa imepangwa kufanyika mwezi ujao. Msemaji wa serikali amewaambia waandishi habari mjini Berlin kwamba Schroeder bado atakutana na rais George W Bush, lakini hatakwenda Carlifornia kwa sababu ya uchaguzi wa mapema unaotarajiwa mwezi Septemba.

Hapo awali kiongozi wa zamani wa chama cha SPD, Oscar Lafontaine, aliyejiuzulu kutoka kwa wadhifa wa waziri wa fedha mwaka wa 1999, alitangaza atakihama chama cha SPD na kuuwakilisha muungano wa upinzani katika uchaguzi ujao. Lafontaine ambaye amekuwa mwanachama wa chama hicho kwa miaka 39, amesema hatua yake hiyo inafuatia mabadiliko ya sheria za wafanyakazi hapa nchini.

Wadadisi wanasema chama kitakachoongozwa na Lafontaine, kitamdhoofisha zaidi kansela Schroeder katika wingi wa kura.