1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Schroeder atangaza mipango ya kuongeza ajira

18 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFW1

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amependekeza kodi za chini kwa makampuni na miradi zaidi ya uchukuzi katika harakati za kuongeza ajira nchini Ujerumani.

Ili kuimarisha mapato Schroeder amesema mianya ya kodi itazibwa na ruzuku kupunguzwa.Mapendekezo yake hayo ni jaribio la kupambana na tatizo sugu la ukosefu wa ajira nchini Ujerumani ambapo watu zaidi ya milioni tano wanajikuta hawana kazi nchini.

Schroeder baadae alikutana na viongozi wa upinzani Angela Merkel na Edmund Stoiber na kusema kwamba wamekubaliana kuunga mkono mipango yake mingi lakini wameipinga mengine kama ule wa kupunguza ruzuku kwa wamiliki wa nyumba.

Hata hivyo kabla ya mazungumzo yao Stoiber alitowa wito wa kuundwa kwa serikali mpya.