1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Schroeder na viongozi wa upinzani wakutana

9 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CETT

Chama cha Social Democrats-SPD na vyama vya kihafidhina CDU na CSU vinakutana leo jioni mjini Berlin kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya Muungano Mkubwa.Mkutano huo unahudhuriwa na Kansela Gerhard Schroeder wa SPD,kiongozi wa chama hicho Franz Münterfering,mgombea wa ukansela wa chama cha CDU,Bibi Angela Merkel na mwenyekiti wa CSU,Edmund Stoiber.Kikwazo kikuu katika majadiliano hayo ya kuunda serikali ya muungano ni suala,nani atakaekuwa kansela.Vyama vya CDU na CSU vinashikilia kuwa Merkel ndio aiongoze serikali mpya.Kwa wakati huo huo chama cha SPD kinamtaka Schroeder aendelee kuwa kansela.Lakini Schroeder binafsi ameonyesha dalili kuwa yupo tayari kuafikiana.Katika uchaguzi wa Septemba 18 hakuna chama cho chote kikuu kilichoweza kupata uwingi mkubwa wa kuweza kuunda serikali mpya.Vyama vya upinzani CDU na CSU vilishinda viti 4 zaidi ya SPD.