1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Serikali ya Ujerumani yatoa ripoti kuhusu usalama wa taifa

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzM

Serikali ya Ujerumani imetoa ripoti rasmi kuhusu usalama wa kitaifa. Ripoti hiyo ya kurasa 133 inaeleza wazi msimamo wa Ujerumani kuhusiana na maswala mbalimbali kama vile biashara huru, ugaidi ndani ya nchi na silaha za maangamizo.

Usalama wa kitaifa, ambao zamani ulikuwa jukumu kubwa la jeshi la Ujerumani, sasa umeorodheshwa nafasi ya tatu kwenye orodha ya mambo muhimu.

Kwa mara ya kwanza serikali ya Ujerumani imefafanua masilahi yake inayotaka kuyalinda katika ngazi ya kimataifa. Ripoti ya serikali inasema kukiwa na dharura, marubani wa jeshi la angani la Ujerumani wataweza kuamriwa kuvurumisha makombora ya kinyuklia ya Marekani.

Ripoti hiyo pia inapendekeza kwamba jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, linaweza kutumwa katika maeneo mbalimbali humu nchini kukabiliana na hali fulani.