BERLIN.Kansela Schröder akutana na baraza lake la mawaziri kujadili kura ya imani
29 Juni 2005Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani leo hii anakutana na baraza lake la mawaziri kuwaeleza sababu za kuitisha kura ya imani ya bunge ijumaa ijayo.
Katika mkutano wa leo makatibu wa dola na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini hawatashiriki katika mazungumzo haya ya siri katika afisi ya kansela mjini Berlin.
Kansela Gerhard Schröder anapendelea ashindwe katika kura ya imani ili rais wa shirikisho Horst Köhler apate kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema.
Malalamiko yanatolewa na baadhi ya wanachama wa serikali kutokana na pendekezo la mwenyekiti wa SPD bwana Franz Münterfering kuwataka wabunge wa vyama vya SPD na walinzi wa mazingira Die GRÜNE wajizuwie kutoa sauti zao.
Wabunge kadhaa wa vyama hivyo viwili wameshaelezea azma ya kuunga mkono kura ya imani kwa kansela.