1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biashara elfu 40,000 Afrika Kusini zimeporwa

21 Julai 2021

Takribani biashara 40,000 nchini Afrika Kusini zimeporwa, kuchomwa moto au kuharibiwa wakati wa ghasia zilizoibuka baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kuanza kutumikia kifungo chake cha miezi 15 gerezani

https://p.dw.com/p/3xmb5
Südafrika , Durban | Plünderungen nahe eines brennenden Warenhauses
Picha: Rogan Ward/REUTERS

Takribani biashara 40,000 nchini Afrika Kusini zimeporwa, kuchomwa moto au kuharibiwa wakati wa ghasia zilizoibuka baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kuanza kutumikia kifungo chake cha miezi 15 gerezani. Serikali ya Afrika Kusini imesema jana kuwa mamia ya maduka na maghala kwenye jimbo la KwaZulu-Natal yaliharibiwa kuanzia Julai 9.

Uvamizi huo ukaeneea hadi Johannesburg, na kusababisha pigo kubwa la uchumi ambao tayari umeathirika na janga la virusi vya corona. Waziri katika Ofisi ya Rais, Khumbudzo Ntshavheni, amewaambia waandishi habari kwamba biashara 40,000 zimeathirika KwaZulu-Natal. Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, jumla ya hasara kwa uchumi wa taifa inakadiriwa kuwa dola bilioni 3.4. Wakati huo huo, jumla ya maduka 90 ya kuuzia dawa yameharibiwa vibaya. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, jana aliwaambia wafanyabiashara kwamba hakuna sehemu yoyote ya uchumi ambayo haijaathiriwa na ghasia hizo.