Biden atangaza msaada mpya wa dola bilioni 2.5 kwa Ukraine
30 Desemba 2024Matangazo
Katika taarifa yake Biden amesema msaada huo mpya utatoa nafasi kwa Ukraine kuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi wake wa anga, silaha na nyenzo zingine muhimu zitakazowasiadia katika uwanja wa mapambano dhidi ya vikosi vya Urusi. Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine unakaribia miaka mitatu na hivi karibuni wanajeshi wa Korea Kaskazini wameungana na vikois vya Urusi katika mapambano dhidi ya vikosi vya Ukraine. Mpaka sasa Marekaniimetoa jumla ya dola bilioni 175 kama msaada wa jumla kwa Ukraine, lakini hakuna uhakika kama misaada itaendelea kwa kasi hiyo chini ya utawala wa Trump, ambaye anachukua nafasi ya Biden mnamo Januari 20. Trump alisema anataka kuvimaliza vita hivyo mara moja.