Daktari wa Biden asema yuko imara kutekeleza majukumu yake
29 Februari 2024Matangazo
Hii ni baada ya rais huyo mwenye umri wa miaka 81 kufanyiwa uchunguzi wa mwisho wa matibabu kabla ya uchaguzi Biden na Trump washinda michujo yao Michigan huku umri wake ukionekana kuwa suala muhimu.
Ripoti hiyo ya uchunguzi wa kila mwaka iliyosubiriwa kwa hamu katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed nje ya mji wa Washington imetolewa wiki chache tu baada ya ripoti ya mwanasheria maalum kumuonyesha kuwa ni mzee na msahaulifu.
Soma pia: Madaktari: Afya ya Biden ni njema
Daktari Kevin O'Connor amesema Biden anaendelea kutekeleza majukumu yake bila matatizo yoyote. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Biden atapambana kwa mara nyingine na Donald Trump mwenye umri wa miaka 77 katika uchaguzi wa Novemba.