Biden aahidi kuilinda Ufilipino kwenye bahari ya Kusini
12 Aprili 2024Matangazo
Biden ametoa ahadi hiyo usiku wa kuamkia leo wakati alipowakaribisha ikulu mjini Washington rais Ferdinand Marcos Jr. wa Ufilipino na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kwa mkutano wa ngazi ya juu wa nchi hizo washirika.
Amesema ahadi ya Marekani ya kutoa ulinzi kwa Japan na Ufilipino ni thabiti na kuongeza kuwa Washington itaisaidia Ufilipino iwapo kutatokea shambulio lolote dhidi ya meli, ndege au vikosi vya nchi hiyo kwenye bahari ya kusini mwa China.
Biden aapa kuzilinda Ufilipino na Japan katikati mwa mvutano na China
Mkutano wa viongozi hao wawatu umefanyika katikati mwa makabiliano yanayoongezeka kati ya meli za Ufilipino na China katika eneo hilo la bahari lenye mzozo ambalo Beijing inadai kulimiliki.