Biden kukutana na Marcos na Kishida kuijadili China
11 Aprili 2024Matangazo
Viongozi hao wanatarajiwa kutangaza kuwa walinzi wa pwani watafanya doria za pamoja katika eneo hilo la kusini mwa Asia mwaka huu. Hii inafuatia mazoezi ya pamoja yaliyofanywa na washirika hao karibu na eneo linalogombaniwa la Bahari ya China Kusini.
Mkutano huo wa kilele unajiri baada ya Biden kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Kishida katika hafla ya heshima ya kidiplomasia inayoashiria kuutambua ushawishi unaoongezeka wa Tokyo kwenye jukwaa la kimataifa.
China ilijibu kwa kusema kuwa Marekani na Japan zinaichafua na kuishambulia Beijing kuhusu masuala ya Taiwan na bahari ya China Kusini, zinaingilia masuala ya ndani ya China na kukiuka kabisa kanuni za msingi zinazosimamia ushirikiano wa kimataifa.