1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Starmer wakutana Washington kuijadili Ukraine

14 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer ameitembelea Ikulu ya White House na kuzungumza na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu hatua zinazofuata katika vita vya Ukraine na Urusi.

https://p.dw.com/p/4kcmu
Joe Biden na Keir Starmer
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer katika ikulu ya White House mjini WashingtonPicha: Manuel Balce Ceneta/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer ameitembelea Ikulu ya White House na kuzungumza na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu hatua zinazofuata katika vita vya Ukraine na Urusi.

Starmer alisema kuwa awamu inayofuata ya Ukraine katika mapigano yake na Urusi inaweza kuwa "muhimu zaidi", huku akiongeza kuwa kwa sasa yapo matukio mengi yaliyopo mbele yao na Marekani pia ikiwa inajiandaa kwa uchaguzi wa rais hapo baadaye mwaka huu.

Soma zaidi. Biden, Starmer waahirisha uamuzi wa makombora ya Ukraine

Lakini licha ya uvumi kabla ya mkutano huo juu ya uwezekano wa mabadiliko ya msimamo wa Marekani na Uingereza kuhusu Ukraine kutumia silaha zao za masafa marefu kushambulia maeneo ya ndani ya Urusi, Marekani ilionesha kutobadili msimamo wake juu ya vita hivyo.

Kwa upande mwingine, Urusi imeonya kuwa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu kutaitumbukiza NATO katika vita vya moja kwa moja na Urusi.