Bilawal Bhutto ateuliwa waziri wa mambo ya kigeni Pakistan
27 Aprili 2022Matangazo
Zardar mwenye umri wa miaka 33 na kiongozi wa chama cha PPP ni mshirika muhimu katika serikali ya mseto ya waziri mkuu Shehbaz iliyoingia madarakani hivi karibuni baada ya kuondolewa kwa utawala wa Imran Khan.
Mwanasiasa huyo kijana kutoka familia ya Bhutto yenye historia pana na siasa za Pakistan atakuwa na dhima ya kurekebisha mahusiano yaliyolegalega kati ya taifa hilo na nchi za magharibi hususani Marekani.
Baada ya kuapishwa Zardar anatarajiwa hii leo kusafiri pamoja na waziri mkuu kwa ziara nchini Saudi Arabia inayolenga kuchochea biashara na uwekezaji.