1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Binti wa Nelson Mandela afariki dunia mjini Johannesburg

13 Julai 2020

Binti wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini na shujaa wa ukombozi Nelson Mandela, Zindzi Mandela amefariki dunia katika hospitali moja mjini Johannesberg.

https://p.dw.com/p/3fEPo
Mandelas Tochter Zindziswa gestorben
Picha: picture-alliance/dpa/AP/M. Dunham

Taarifa hizo zimetolewa na msemaji wa chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress ANC siku ya Jumatatu. Zindzi Mandela ambaye mama yake alikuwa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, Winnie Madikizela Mandela alipata umaarufu kimataifa aliposoma waraka wa Nelson Mandela wa kukataa kuachiwa huru mwaka 1985 kwa pendekezo la aliyekuwa wakati huo rais wa Afrika Kusini P.W Botha. Botha aliahidi kuamuchia huru Mandela kwa sharti la kupinga matumizi ya nguvu kama silaha ya kisiasa. Shirika la utangazaji la taifa SABC limesema binti huyo wa Mandela mwenye umri wa miaka 59 ambaye alikuwa ni balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark amefariki katika hospitali mjini Johannesberg ingawa ugonjwa uliomuuwa haukutajwa. Msemaji wa chama cha ANC, Pule Mabe amesema maelezo zaidi yatatolewa kadri muda unavyokwenda.