SiasaUingereza
Blinken na Starmer kujadili namna ya kuisaidia Ukraine
10 Septemba 2024Matangazo
Katika mkutano huo utakaofanyika London, viongozi hao watajadili pia kuhusu namna ya kukabiliana na mzozo wa Mashariki ya Kati.
Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Blinken atajadiliana pia na Waziri Mkuu Stammer na Waziri wa Mambo ya Kigeni David Lammy kuhusu ukanda wa Indo-Pasifiki na mkataba wa ulinzi wa AUKUS kati ya Marekani, Australia na Uingereza.
Ziara ya Blinken nchini Uingereza inafanyika baada ya afisa wa juu wa Iran kukanusha ripoti kuwa Tehran iliipa Urusi makombora ya masafa marefu, Umoja wa Ulaya ukisema taarifa hiyo ni ya kuaminika.