Blinken azungumza na viongozi wa Armenia na Azerbaijan
29 Aprili 2024Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema kuwa Blinken alizungumza jana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na kumhimiza kuendeleza juhudi zake za mazungumzo na mwenzake waArmeniahuku akikariri kujitolea kwa nchi hiyo katika kuunga mkono juhudi hizo.
Soma pia:Azerbaijan, Armenia mbioni kufikia makubaliano ya amani
Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Aliyev, Blinken pia alipongeza hatua ya kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa mchumi mmoja maarufu wa Azerbaijan ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani aliyekuwa amefungwa tangu Julai mwaka jana akisubiri kesi dhidi yake.
Marekani yasisitiza kuunga mkono mazungumzo ya amani kati ya Armenia na Azerbaijan
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imesema, katika mazungumzo tofauti na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, Blinken alisisitiza uungaji mkono wa Marekani kwa ufanisi wa makubaliano ya amani ya kudumu na ya heshima, lakini haikufafanua siku yalipofanyika mazungumzo hayo.