Blinken aitaka Mashariki ya Kati kujizuia kuongeza mzozo
1 Agosti 2024Akizungumza katika mji mkuu wa Mongolia, Blinken alionya kwa kusema Mashariki ya Kati inaelekea kwenye mzozo zaidi, machafuko, mateso na kukosekana usalama, na kuongeza kuwa ni muhimu mzunguko huu ukavunjwa.
"Antony Blinken: Na ili kufika hapo, kwanza inatakiwa pande zote kuachana na matukio ya uchochezi. Pia wanatakiwa kusaka sababu ya kukubaliana, na si sababu ya kuchelewesha ama kuyakataa makubaliano. Na ni muhimu kwamba pande zote zifanye maamuzi sahihi katika siku zijazo."
Soma pia: Baraza la Usalama la UN laijadili hali ya Mashariki ya Kati
Kifo cha kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh kilichotokea masaa kadhaa baada ya Israel kusema imemuua kamanda wa juu wa Hezbollah, vinachukuliwa kuuchochea mzozo katikati ya wasiwasi mkubwa unaozidishwa na vita vya Gaza.