Blinken amuhimiza Netanyahu kuruhusu misaada Gaza
7 Februari 2024Matangazo
Akizungumza baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Blinken alisema hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa mbali na kuwasilishwa kwa misaada, ndilo lengo hasa la ziara na mikutano yake.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ameonesha matumaini kuhusiana na suala la makubaliano ya kuwaachia mateka walio mikononi mwa wanamgambo wa Hamas, ila akasema kuwa juhudi zaidi zinahitajika.
Haya yanafanyika wakati ambapo jeshi la Israel likisema kuwa limegundua na kuliharibu handaki linalotumiwa na viongozi wa kundi la Hamas kuwashikilia mateka katika mji muhimu wa Gaza wa Khan Younis.
Jeshi hilo linasema handaki hilo lina urefu wa zaidi ya kilomita moja.