1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken yuko Israel katika ziara yake ya 11 baada ya vita

22 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Israel mapema hii leo katika ziara yake ya 11 katika eneo hilo tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4m57D
Laos | ASEAN-US Gipfel Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akizungumza katika Mkutano wa 12 wa ASEAN mjini Vientiane, Laos Oktoba 11, 2024.Picha: TANG CHHIN SOTHY/via REUTERS

Mwanadipiplomasia huyo wa Marekani anatarajiwa kukutana na maafisa wakuu wa Israel ili kujadili namna ya kufufua  juhudi za kusitisha mapigano katika ukanda huo baada ya mauaji ya kiongozi mkuu wa Hamas Yahya Sinwar. Blinkenalitua saa chache baada ya Hezbollah kufyatua roketi kadhaa za mashambulizi katikati mwa Israel leo ingawa mpaka sasa hakuna taarifa za uharibifu au majeraha zilizoripotiwa. Wakati huo huo, Jeshi la Israeli limesema takriban makombora 15 yalirushwa kutoka Lebanon hadi kaskazini mwa Israeli. Mashambulizi hayo yanajiri wakati Israel ilipoyashambulia maeneo ya kusini mwa Lebanon ambapo imesema ilikuwa ikilenga taasisi ya fedha inayoendeshwa na Hezbollah.