1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken ziarani Uingereza kujadili mizozo ya Ukraine na Gaza

10 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili Uingereza kwa ziara itakayojumuisha mazungumzo mapana na serikali ya nchi hiyo ambayo yanatarajiwa kugusia vita vya Ukraine na mzozo wa Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4kRVW
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken.Picha: Roberto Schmidt/Pool/AP Photo/picture alliance

Akiwa mjini London anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer na Waziri mwezake wa mambo ya nchi za nje Matthew Miller.

Ziara yake inafanyika siku kadhaa kabla ya Starmer kuitembelea Marekani kwa mazungumzo na Rais Joe Biden mjini Washington. Kiongozi huyo atasafiri siku ya Ijumaa kwenda Marekani kwa mkutano na Rais Biden ambao utakuwa wa pili tangu chama chake cha Labour kiliposhinda uchaguzi mwezi Julai.

Marekani na Uingereza zinashirikiana kwenye masuala yote makubwa ya kimataifa, na Starmer ameweka wazi azma yake ya kuendelea kuimarisha nafasi ya Uingereza ya kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Serikali yake pia imechukua msimamo madhubuti dhidi ya Israel ikiishinikiza kufanya inaloweza kupunguza madhila ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza.

Serikali ya Starmer pia imezuia baadhi ya mauzo ya silaha kwa Israel ikisema ina wasiwasi zinaweza kutumika kukiuka sheria za kimataifa.