BLINTIRE: Serikali ya malawi yatowa mwito wa kupewa misaada ya vyakula-
15 Januari 2004Matangazo
Serikali ya Malawi, imetowa mwito wa kupewa msaada wa vyakula, kwa ajili ya raia wake zaidi ya miliyoni tatu na nusu, wanakabiliwa na njaa.
Waziri wa kilimo Chakufwa Chihana amesema zaidi ya asilimia thelathini na mbili ya raia miliyoni kumi na moja wa Malawi, hawana chakula, na ikiwa jamii ya kimataifa haitaingilia kati, basi watu hao watakuwa hatarini.
Waziri huyo amesema hali hiyo imetokana na ukame uliokuwepo kwa zaidi ya miaka miwili, na wataalamu wanasema mvua ambazo zilitarajiwa kunyesha tangu mwezi september, wakati huo ndipo zinaanza kunyesha, na kwa viwango vya chini kabisa katika baadhi ya maeneo ya Malawi, kiasi kwamba hata mwaka huu wa 2004, wakulima wa Malawi hawawezi kutarajia mavuno.