Bobi Wine azindua chama kipya cha siasa kabla ya uchaguzi
22 Julai 2020Mwanaharakati wa Uganda Bobi Wine amezindua chama kipya cha siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa rais ambamo ana matumaini kuwa taswira ya umoja wa upinzani dhidi ya rais wa muda mrefu nchini humo Yoweri Museveni.
Mwanamuziki huyo maarufu nchini Uganda na mbunge, ambaye jina lake halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, ameongoza kundi la kutoa shinikizo la kisiasa linalojulikana kama People Power, ikiwa na maana ya Nguvu ya Umma, ambalo limevutia hisia za Waganda wengi kwa wito wake wa kutaka rais Yoweri Museveni kung'atuka.
Wine amekiita chama chake kipya National Unity Platform, ama Jukwaa la Umoja wa Taifa, na mwamvuli ikiwa ndio nembo yake. Amekuwa akitoa wito wa umoja wa upinzani dhidi ya Museveni, mshirika wa marekani katika usalama wa kikanda ambaye ameliongoza taifa hilo la Afrika mashariki tangu kuchukua madaraka kwa njia ya kijeshi mwaka 1986.