MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Bomu laua watu 12 wakiwemo watoto nchini Kongo
4 Mei 2024Matangazo
Msemaji wa shirika la kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Jean Jonas Yaovi Tossa, amesema watu wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo. Msemaji wa jeshi la Kongo, Luteni Kanali Ndjike Kaiko, alilituhumu kundi la waasi wa M23 kuhusika na mashambulizi hayo.
Lakini kundi hilo limezitupilia mbali tuhuma hizo. Rais Felix Tshisekedi aliyeko ziarani barani Ulaya ametangaza kusitisha ziara hiyo na kurejea nyumbani.
Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, amelaani mashambulizi hayo na kuilaumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.
Marekani imetoa wito kwa pande husika kusitisha mapigano na kuheshimu sheria za kimataifa ya juu ya haki za binadamu.