1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boris Johnson ang'aa kumrithi May

19 Juni 2019

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amedhihirisha umadhubuti wake katika nafasi ya kuwa kiongozi wa chama cha Conservative, akitarajiwa kumrithi waziri mkuu wa sasa,Theresa May.

https://p.dw.com/p/3KhHW
Boris Johnson vor Downingstreet 10
Picha: picture-alliance/dpa/H. Mckay

Boris Johnson ameibuka na ushindsi wa kura 126 kati ya kura 313 katika duru hii ya pili ya uchaguzi iliyofanyika  iliyofanyika Jumanne, ambayo inahusisha wagombea sita wenye kuwania nafasi ya kumrithi waziri Theresa May kwa nafasi ya uongozi wa chama. Aliyemfuatia katika mchuano huo alikuwa waziri wa mashauri ya kigeni wa sasa Jeremy Hunt aliepata kura 46 tu.

Hunt anakwenda katika duru ya inayofuta ya uchaguzi akiwa sambamba waziri wa mazingira Michael Gove,waziri wa mambo ya ndani Sajid Javid na Rory Stewart. Katika duru hiyo aliyekuwa waziri wa mpango wa Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya Brexit Dominic Raab aliondolewa. Jumapili iliyopita mwamba wa kushinikiza Brexit, alionekana madhubuti katika mdahalo wa televisheni mbele ya wagombea wenziwe wanne katika mjadala huo.

Mdahalo haukuwa na mshindi

England: Boris Johnson Michael Gove
Wagombea Boris Johnson na Michael GovePicha: picture-alliance/S. Rousseau

Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza hakukuwa na mshindi wa wazi baada ya mjadala husika, ambao ulijikita katika masuala ya Brexit, chuki dhidi ya Uislamu na mabadiliko ya tabia nchi. Johnson, aliejizolea umaarufu katika kampeni ya Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ya kabla ya kura ya maoni ya 2016, alirejea ahadi yake ya misimamo mikali ya majadiliono na umoja huo na alisisitiza uwezekano wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kuwa ni jambo lililo wazi kabisa kwake.

Jonhson alisema Uingereza inakabiliwa na jamngo kupoteza imani yake katika siasa endapo muda mpya wa mwisho uliopangwa wa kujiondoa katika umoja wa ulaya wa Okotab 31 hautatekelezwa. Katika duru ya kwanza ya upigaji kura ya Jumanne, Johnson alipata uungwaji mkono wa kura 114 kati 313 za wabunge.

Kwa mujibu wa utaratibu wa uchaguzi huo mgombea alipaswa kupata uungwaji mkono wa takribani wabunge 33. Chaguzi zaidi zitaendelea juma hili, mpaka wapatikane wagombea wawili.Baadae wanachama wa 160,000 wanatarajiwa kuwapigia wagombea hao kuchagua mshindi, na matokoe yake kutarajiwa kutolewa katika juma linaloanza tarehe 22 mwezi ujao. Maafisa wengi walijiuzulu Juni 7 baada ya kuishindwa kupata ridhaa ya bunge kwa  Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya.

Chanzo DPAE