1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borrell:Sitarajii mafanikio makubwa kuhusu biashara huria

17 Julai 2023

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema leo kuwa hatarajii hitimisho la haraka la makubaliano yanayotarajiwa ya biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya, Brazil, Argentina, Uruguay na Paraguay.

https://p.dw.com/p/4U0f4
Geberkonferenz der EU für Syrien
Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP/dpa/picture alliance

Akizungumza mjini Brussels, kabla ya mkutano wa kwanza wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, Caribbean na Amerika ya Kusini baada ya miaka minane, Borrell amesema kuwa hatarajii mafaniko makubwa na kuongeza kuwa anatarajia pande zote kufanya kazi kufikia muafaka mwishoni mwa mwaka.

 Soma pia:Umoja wa Ulaya waondoa vikwazo vya vyakula vya Japan


Mkataba wa biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na Soko la Pamoja la Kusini (MERCOSUR) umesimama tangu kumalizika kwa mazungumzo mnamo 2019.

Baadhi ya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yalikuwa yameomba kuongezwa kwa masuala kuhusu hali ya hewa, mazingira na haki za binaadamu lakini mataifa ya Amerika Kusini yamekosoa pendekezo hilo.