1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bradley Manning wa WikiLeaks mahakamani

Sonila Sand3 Juni 2013

Mwanajeshi wa Marekani aliyekabidhi nyaraka za siri za serikali ya Marekani kwa mtandao wa WikiLeaks, Bradly Manning anafikishwa mahakani, zaidi ya miaka mitatu baada ya kukamatwa nchini Iraq. Je, ni shujaa au msaliti?

https://p.dw.com/p/18inM
Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumuunga mkono Bradly Manning.
Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumuunga mkono Bradly Manning.Picha: Reuters

Kwa Heather Linebaugh mwenye umri wa miaka 24, Bradly Manning ni shujaa, ambae aliwasaidia wamarekani kufahamu kinachoendelea katika uwanja wa kivita.Linebaugh alikuwa mmoja wa mamia ya waandamanji waliohimili jua kali siku ya Jumamosi mchana, na kusimama mbele ya kambi ya kijeshi ya Fort Meade, katika mji wa Maryland, kuonyesha mshikamano na Manning, huku wakiimba nyimbo za "Muachieni huru Bradly Manning", "ukweli uko upande wetu" na "Bradly Manning siyo msaliti."

Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumuunga mkono Bradly Manning, mbele ya kambi ya kijeshi ya Fort Meade, ambako kesi yake inaanza kusikilizwa. Demonstrationszug entlang der Kaserne Fort Meade, auf das Kasernengelände selbst durften die Demonstranten nicht Bild: DW/Christina Bergmann, Fort Meade, Maryland, USA, 1.6.2012
Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumuunga mkono Bradly Manning, mbele ya kambi ya kijeshi ya Fort Meade, ambako kesi yake inaanza kusikilizwa.Picha: DW/C. Bergmann

Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 25 na mwenye cheo cha Koporo anatuhumiwa kuwa wakati akiwa kwenye kituo chake cha kazi nchini Iraq, alihamisha taarifa za siri za jeshi la Marekani na wizara ya mambo ya kigeni kutoka kwenye computer na kuzitoa kwa mtandao wa WikiLieaks. Hapo awali alishtakiwa kwa ujasusi na kumsaidia adui, hasa kundi la Alqaeda na kiongozi wake Osama Bin Laden, na anakabiliwa na kifungo cha maisha iwapo atatiwa hatiani. Lakini mwenyewe amekanusha mashtaka hayo.

Akiri baadhi ya makosa

Katika mashtaka 10 kati ya 22 Bradly alikiri kuwa na hatia na anaweza kufungwa jela miaka 20. Lakini anakanusha mashtaka ya kufanya ujasusi na kumsaidia adui. Pamoja na kutuma taarifa za siri za kidiplomasia kuhusiana na operesheni za Marekani nchini Iraq na Afghanistan, Manning pia alitoa mkanda wa video ukionyesha shambulio la helikopta dhidi ya raia nchini Iraq, likifanywa na wanajeshi wa Marekani, ambamo pia waandhishi wawili wa habari waliuawa.

Heather Linebaugh ambae aliwahi kufanya kazi kama ya Manning, akichambua taarifa na video za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, anasema video hiyo iliyotolewa na Manning inabainisha wazi hali katika uwanja wa vita ncnini Iraq, ambako raia wasio na hatia wamekuwa wahanga wa vita hivyo. Nathan Fuller, msemaji wa mtandao unaomuunga mkono Manning ambao uliandaa maandanamano mbele ya kambi ya Fort Meade anasema Manning alihatarisha maisha yake kwa ajili yao.

"Alihatarisha maisha na uhuru wake kwa kiasi kikubwa kwa ajili yetu, kutufahamisha nini serikali yetu inakifanya kwa siri, na tunadhani anahitaji msaada na utetezi wetu," anasema Fuller.

Muazilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange, ambae bado amejificha kwenye ubalozi wa Equador mjini London Uingereza
Muazilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange, ambae bado amejificha kwenye ubalozi wa Equador mjini London UingerezaPicha: dapd

Mawakili wake wamefanikiwa kuishawishi mahakama kuwa Manning alipata manyanyaso kutoka kwa maafisa wa kijeshi wa marekani, ikiwa ni pamoja na kuwekwa katika kifungo cha upweke kwa zaidi ya mwaka mmoja, wakati mwingine akiwa amevuliwa nguo. Kutokana na hoja hiyo, atapunguziwa siku 112 katika kifungo chochote atakachohukumiwa

Sio wa kwanza kuvujisha siri

Lakini Daniel Ellsberg, mwenye umri wa miaka 82 na ambae aliwahi kushtakiwa miaka ya 1970 kwa kosa kama la Manning, alipotoa taarifa za siri kuhusiana na vita vya Vietnam, anasema mateso aliyoyapta Manning ni sababu tosha ya kufutwa kwa kesi hiyo.

"Naungana na Bradly Manning kwa kiasi kikubwa. Hakuna ushahidi wowote uliotolewa unaoweza kuhatarisha majeshi ya Marekani wala mtu yeyote na hii ni aibu kubwa kwa serikali," anasema Ellsberg ambae alivujisha taarifa kwamba serikali ilikuwa inafahamu kuwa haiwezi kushinda vita vya Vietnam wakati inakwenda huko, na kwamba ilikuwa ikitoa taarifa zisizo na ukweli kuhusiana na idadi ya vifo katika vita hivyo.

Kwa Nathani Fuller mwenye umri wa miaka 24, kumuunga mkono Manning imekuwa kazi yake kamili kwa sasa, kwa sababu kesi hiyo itaendelea kwa muda wa wiki 12. Na wanapanga kufanya maandamano ya mshikamano na Manning kwa wakati wote huo.

Mwandishi: Bergmann Christina (DW Washington)
Tafisiri: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Josephat Nyiro Charo