1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil imeifunga Korea Kusini, na Croatia Japan

6 Desemba 2022

Katika michezo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Brazil imeinyuka Korea Kusini mabao 4 kwa 1.Na Croatia imeiondoa uwanjana Japan baada ya kuibuka na ushindwa mikwaju mitatu ya penalti, huku Japan ikiambulia mmoja.

https://p.dw.com/p/4KW62
FIFA Fußball WM 2022 Katar | Brasilien - Südkorea
Picha: Heuler Andrey/Action Plus/picture alliance

Kwa hatua hiyo sasa Brazil itakabiliana uso kwa uso Croatia katika ngwe ya robo fainali. Mchezaji ghali kabisa Neymar ambae aliwekwa kando katika mechi mbili za kombe la dunia za timu hiyo kutokana na kuwa na maumivu ya mguu alionekana kurejea katika nafasi yake.

Ndani ya kipindi cha dakika 7 tu mchezaji Vinicius Junior aliweka kimyani bao la ufunguzi, kabla ya Neymar kufanya hivyo, hatua ambayo inamfikisha magali 76 kwa kuifungia timu yake ya taifa akiwa nyuma ya goli moja kuvunja rekodi aliyoiweka nguli wa soka wa Brazil, Pele.

Pele aangalia soka akiwa kitandani Brazil

FIFA Fußball WM 2022 Katar | Brasilien - Südkorea
Washabiki wa soka wa Brazil na bendera ya PelePicha: Ariel Schalit/AP/picture alliance

Pele mwenyewe mwenye umria wa miaka 82 ambae kwa sasa ni mgonjwa alikuwa akikiangalia kipute hicho akiwa hospitalini mjini Sao Paulo, ambako alipelekwa tangu Jumanne iliyopita akiendelea na matibabu ya ugonjwa wa saratani ya utumbo. Bila shaka alifurahishwa na bao la Richarlison likiwa bao la tatu kabla ya lile la Lucas Paqueta ambayo yote kwa nyakati tofauti yalifungwa kabla ya kipindi cha pili cha mchezo.

Kwa upande wa Korea Kusini aliyewafungua gili la kufuta machozi ni Paik Seung-ho. Lakini kwa Brazil ni mara ya kwanza kuibuka na ushindi wa magoli manne tangu mwaka 1998.

Na katika mchuano wa awali Croatia imesogea katika hatua ya robo fainali baada ya kuichapa Japan katika ngwe ya mikwaju wa penalti.

Timu zote mbili zilikuwa na nguvu sawa uwanjani

FIFA Fußball WM 2022 in Katar | Kroatien - Japan
Wachezaji wa CroatiaPicha: Adrian Dennis/AFP/Getty Images

Timu zote mbili zilionekana kumyenyana vikali katika ngwe zote hatua ambayo ilihitimisha kwa kutoshana nguvu kwa mabao ya moja kwa moja. Daizen Maeda ndio alipiga bao la kifungua kinywa kwa upande wa Japan, kitendo ambacho kilifanyika katika dakika ya 43. Na Croatia aliewafuta machozo ni Ivan Perisic, akisawazisha katika dakika ya 55.

Lakini Croatia ilisonga mbele katika hatua ya penalti kwa kuichapa Japan mabao matatu kwa moja, pale ambapo magali ya Nikola Vlasic, Marcelo Brovic na Mario Pasalic. Takuma Asano aliipatia bao Japan, lakini kipa wa Croatia Dominic Kivakovic aliweza kuyadhibiti vyema majaribio ya Takumi Minamino, Kaoru Mitoma na Maya Yoshida.

Soma zaidi:Ni Japan au Croatia kuingia robo fainali?

Leo hii ni Morocco na Uhispania, Ureno na Uswisi, zingatia la Afrika litakuwa Morocco baada ya kipigo cha bao tatu kwa sifuri cha Senegal kutoka kwa England.