1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Atakaye chukua uongozi wa IMF atajadiliwa kesho.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkT

Nafasi ya mkuu mpya wa shirika la fedha la kimataifa inaonekana kutoweza kukubaliwa katika mkutano wa mawaziri wa fedha wa umoja wa Ulaya utakaofanyika siku ya Jumanne.

Mataifa ya Ulaya yanatafuta mtu atakayechukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa sasa wa IMF, baada ya raia huyo wa Hispania Rodrigo Rato kusema hivi karibuni kuwa anataka kujiuzulu ifikapo mwezi wa Oktoba.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wiki iliyopita amependekeza jina la waziri wa zamani wa fedha wa Ufaransa Dominique Staruss-Kahn kuchukua wadhifa huo. Hata hivyo , duru ndani ya uongozi wa Ureno katika umoja wa Ulaya zinasema kuwa anatarajia mabadilishano ya wazi ya mawazo kuhusiana na suala hilo katika mkutano huo wa kesho na hakuna jina moja ambalo limekwishakubaliwa.

Kwa kawaida , Ulaya inaongoza shirika la IMF na Mmarekani anaongoza benki kuu ya dunia.