1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Hakuna maafikiano kuhusu bajeti ya Umoja wa Ulaya

18 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF2R

Viongozi wa Umoja wa Ulaya,wameshindwa kukubaliana juu ya bajeti ya Umoja huo.Waziri mkuu Jean-Claude Juncker wa Luxembourg, amethibitisha kuwa mkutano wa kilele haujafanikiwa kuleta maafikiano.Juncker akionyesha masikitiko amesema,Ulaya inajikuta katika mgogoro mkubwa.Waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair amesema,Uingereza haitokubali kupunguziwa nafuu ya mabilioni ya Euro inazopata kila mwaka,ila kama punguzo hilo litakwenda sambamba na mageuzi ya ruzuku za kilimo katika Umoja wa Ulaya,jambo ambalo hasa linakataliwa na Ufaransa.Luxembourg,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka,imeshauri kuwa suala la punguzo liahirishwe kwa hivi sasa,lakini Uingereza, Uholanzi,Hispania,Sweden na Finnland zimeupinga mpango huo.