BRUSSELS: Uturuki isishambulie waasi ndani ya Irak
16 Oktoba 2007Matangazo
Mpango wa Uturuki kutaka kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Kikurd ndani ya ardhi ya Irak unazidi kulaumiwa.Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia wakimbizi,Antonio Guterres akizungumza mjini Brussels amesema, hatua kama hiyo itasababisha wimbi la wakimbizi katika kanda ya utata.Umoja wa Ulaya na Marekani kwa mara nyingine tena,zimetoa mwito kwa Uturuki iliyo mshirika wao katika NATO,kutochukua hatua ya kijeshi,kaskazini mwa Irak.