1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Maadhimisho ya siku ya Maji Ulimwenguni yaanza

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGq

Washiriki katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Maji Ulimwenguni wanakutana mjini Brussels nchini Ubelgiji wiki hii wanatoa wito kwa maji kutambuliwa kama haki ya kimsingi na umiliki wake kutoachiwa makampuni binafsi.

Ikiwa siku moja kabla siku ya kuadhimisha maji Ulimwenguni,maafisa teule,mashirika yasiyo ya serikali wanasisitiza kuwa maji ni chanzo cha mizozo ya kiuchumi vilevile mikakati.

Umoja wa mataifa unakisia kuwa ifikapo mwaka 2025 thuluthi mbili ya watu ulimwenguni itakabiliwa na matatizo ya maji.Maeneo ambayo huenda yakaathiriwa zaidi ni Afrika kaskazini,Mashariki ya kati vilevile magharibi mwa Asia.

Kulingana na wataalam ongezeko la joto ulimwenguni linachangia kwa kiasi kikubwa katika uhaba wa maji.

Asilimia 90 ya maji ya ulimwengu yanamilikiwa na serikali ila hilo halitoshi kulingana na washiriki wa mkutano huo.Washiriki hao kwa upande mwingine wanadai kuwa bei ya kutoa huduma za maji ni ya chini sana jambo ambalo halivutii wawekezaji binafsi katika sekta hiyo.

Baraza la maji la Ulimwengu linakisia kuwa chini ya dola bilioni 66 kwa mwaka zinatumika kwa mwaka kutoa huduma za maji kwa wakazi wanaohitaji maji safi na salaama.Baraza hilo linapendekeza kuongeza kodi ya safari za ndege,bustani vilevile mataifa tajiri yaliyo na maji kwa wingi ili kugharamia utoaji wa huduma hiyo.