Brussels.Uchunguzi waamuriwa juu ya kukatika kwa Umeme katika nchi za Ulaya.
6 Novemba 2006Matangazo
Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imetaka uchunguzi ufanyike juu ya chanzo kilichosababisha kukosekana kwa umeme katika sehemu kadhaa za Ulaya Magharibi na kusema kuwa, inapendekeza hatua mpya zichukuliwe mwakani ili kuondokana na tatizo kama hilo.
Wakati huo huo Kampuni ya umeme ya Ujerumani E.ON imekubali lawama kuwa inahusika na ukatikaji huo wa umeme na kusema, nguzo yake ya umeme ilizidiwa na wingi wa umeme, baada ya kuuzima umeme upande wa mto Ems ili kuiruhusu meli kupita kwa usalama.
Kukatika kwa umeme huo kulipelekea mamilioni ya watu kukosa umeme katika nchi za Ujerumani, Ufaransa, Italy, Hispania na Ureno.
Licha ya hasira za wanasiasa kampuni ya E.ON imesema mfumo wa waya wa umeme wa Ulaya upo katika hali nzuri.