BUJUMBURA:Burundi kupata msaada wa Benki ya Dunia
7 Machi 2007Benki ya Dunia inapanga kuipa nchi ya Burundi msaada wa dola bilioni laki moja thelathini kuisaidia kujijenga na kudumisha amani kufuatia kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Fedha hizo zinapangiwa kuimarisha uchumi,huduma za elimu vilevile miradi ya nishati kulingana na Mkuu wa Benki hiyo Paul Wolfowitz.
Nchi ya Burundi imetatizwa na uhasama kati ya makabila mawili makuu nchini humo ya Wahutu walio wengi na Watutsi waliokuwa na nafasi nyingi za uongozi tangu kupata uhuru kutoka kwa nchi ya Ubelgiji mwaka 62.Vita nchini humo vilianza mwaka 93 pale wanajeshi wa miavuli wa Kitutsi walipomuua Rais wa kwanza aliyeteuliwa kwa misingi ya kidemokrasia Melchior Ndadaye.Uchaguzi wa mwaka 2005 ulisababisha uongozi mpya na Pierre Nkurunziza kushinda na kuteuliwa kuwa rais wa nchi hiyo.