1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga: Dirisha la uhamisho

22 Julai 2024

Dirisha kuu la uhamisho wa wachezaji Ulaya lipo wazi, tutazame wanaohama na kujiunga na ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga.

https://p.dw.com/p/4ibNk
Kombe la ubingwa wa Bundesliga DFB
Kombe la Bundesliga. Litatua wapi msimu wa 2024-2025? Picha: Burghard Schreyer/kolbert-press/IMAGO

Bayern Munich imesajili wachezaji watatu muhimu katika azma yao ya kutafuta tena taji la Bundesliga, wakati mabingwa watetezi Bayer Leverkusen wakiendelea kujipanga ili kuimarisha kikosi chake.

Miongoni mwa waliojiunga na Bundesliga ni pamoja na Kamil Grabara mlinda lango anayejiunga na Wolfsburg, kuchukua nafasi za kipa mzoefu Koen Casteels.

Leverkusen wamemchagua beki wa kati wa Ufaransa wa kikosi cha wachezaji chini ya miaka 19 Jeanuël Belocian kuwa miongoni mwa wachezaji wapya walioongezwa kwenye kikosi chao kilichotwaa ubingwa. Kinda huyo anajiunga akitokea Stade Rennes, ambako alicheza mechi 32 za ligi msimu uliopita na mechi sita zaidi akijumuishwa kwenye mechi za ligi ya Ulaya.

Soma pia: Leverkusen haitikisiki kileleni mwa Bundesliga

Aleix García, Baada ya msimu wa kihistoria nchini Uhispania akiwa na Girona, waliofuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao, García ameamua kujiunga na Mhispania mwenzake aliyeweka historia Ujerumani, Xabi Alonso, kocha wake mpya ndani ya kikosi cha Bayer Leverkusen.

Bayern Munich nayo imeamua kumsajili raia wa Japan Hiroki Ito akitokea klabu ya Stuttgart baada ya kudhihirisha uwezo mkubwa ndani ya MHPArena.

Michael Olise vile vile anatua Bayern baada ya kuonyesha ufundi, utulivu na vyenga vingi wakati  Bavarians wakipania kutwaa tena taji la Bundesliga.

João Palhinha kiungo wa kati wa Ureno naye pia anajiunga na kikosi cha Vincent Kompany akiwa na kiwango kizuri katika klabu ya vijana ya Sporting Lisbon.

Sura mpya, msimu mpya

Utambulisho wa kocha mpya FC Bayern, Vincent Kompany
Vincent Kompany kocha mpya wa Bayern Munich.Picha: Sven Hoppe/picture alliance/dpa

Miongoni mwa sura mpya katika bundesliga msimu ujao ni Can Uzun mchezaji mwenye umri wa miaka 18 anayewasili Eintracht Frankfurt akiwa amejijengea jina katika Bundesliga daraja la 2 akiwa na Nuremberg. Kwa mashabiki wa Frankfurt, sasa wanaweza kuwa na matumaini na mshambuliaji wao mpya kijana, mwenye shauku na mbunifu.

Mchezaji Assan Ouédraogo ingawa bado ana umri wa miaka 18 tu, kuna matarajio mengi kwenye mabega ya nyota mpya wa Leipzig. Ouédraogo, ambaye babake ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Burkina Faso, amekuwa akitamba katika Ligi ya Bundesliga tangu alipocheza kwa mara ya kwanza Bundesliga daraja la pili 2 kwa Schalke.

Borussia Dortmund hawakuachwa nyuma katika usajili, baada ya kuondoka kwa Mats Hummels, wamemsajili Waldemar Anton, kujaza pengo lililoachwa Hummels akitokea VfB Stuttgart.

Soma pia: Guirassy avunja rekodi za Bundesliga

Baada ya kutamba na kungara kwenye bundesliga msimu uliopita, mshambuliaji wa timu ya tiafa ya Guinea Serhou Guirassy anajiunga na Dortmund baada ya kumwaga wino kwenye mkataba wa miaka minne na klabu hiyo.