1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haitotuma makombora ya masafa marefu Ukraine

14 Machi 2024

Wabunge wa Ujerumani kwa mara nyengine wameukataa wito wa upinzani unaoitaka serikali kuipelekea Ukraine makombora ya masafa marefu ya Taurus, siku moja baada ya kansela Olaf Scholz kuutetea msimamo wake huo.

https://p.dw.com/p/4dWna
Bunge la Ujerumani, Bundestag
Wabunge wa Ujerumani wakataa kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu ya TaurusPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Bunge la Ujerumani, Bundestag, limeukataa muswada huo wa upinzani kwa kura 495 kwa 190 huku kukiwa na wabunge watano ambao hawakuwepo kushiriki kura hiyo.

Upinzani ulikuwa unataka kuendelea kushinikiza kuhusiana na suala hilo na kutumia mgawanyiko ulioko katika serikali ya muungano ya Kansela Scholz.

Scholz asisitiza msimamo wake wa kutoipa Ukraine makombora ya Taurus

Hapo jana Scholz aliwaambia wabunge kwamba kukataa kwake kuchukua hatua hiyo hakumaanishi kwamba haiamini serikali ya Kyiv.

Hayo yakiarifiwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, ameyataka mataifa rafiki kwa Ukraine katika jumuiya hiyo ya kujihami, kuipelekea silaha nchi hiyo. Stoltenberg amesema kuna haja ya dharura ya Ukraine kupelekewa silaha katika vita vyake na Urusi.