Bunge la Ulaya lamtunuku Mahsa Amini tuzo Uhuru ya Sakharov
19 Oktoba 2023Matangazo
Rais wa Bunge hilo, Roberta Metsola, amesema wanaendelea kusimama kwa fahari na watu jasiri ambao wanapigania usawa, utu na uhuru nchini Iran.
Mahsa Amini, ambaye alikuwa na umri wa miaka 22, alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi wa maadili, baada ya kuzuiliwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi.
Soma zaidi: Iran: Waandamanaji waadhimisha mwaka mmoja wa ukandamizaji wa vikosi vya usalama Zahedan
Kifo chake kilisababisha maandamano makubwa katika taifa hilo la Kiislamu.
Tuzo ya Sakharov imekuwa ikitolewa na Bunge la Ulaya tangu 1988 kwa watu binafsi na mashirika ambayo yamekuwa yakitetea haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Mwaka jana tuzo hiyo ilitolewa kwa watu wa Ukraine kwa kutetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi.