Burkina Faso yaidhinisha muswaada wa kutuma kikosi Niger
31 Agosti 2023Jumuiya hiyo inayotaka kurudisha utawala wa kiraia kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoonekana leo Alhamisi, muswaada huo uliidhinishwa katika mkutano wa viongozi wa serikali, inayohodhiwa na majenerali.
Hata hivyo taaarifa hiyohaikutowa ufafanuzi kuhusu hatua za kutumwakikosi hicho ingawa imeweka wazi kwamba maamuzi yaliyofikiwa yanatokana na makubaliano ya pamoja kati ya nchi hizo mbili BurkinaFaso na Niger.
Soma pia:Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuiwekea viongozi Niger
Taarifa hiyo pia ilimnukuu waziri wa ulinzi wa Burkina Faso Kasssoum Coulibaly aliyesema kwamba kile kinachoathiri usalama ndani ya Niger kimsingi kinaathiri pia usalama ndani ya Burkina Faso.
Muswaada huo sasa utawasilishwa katika bunge la mpito la nchi hiyo ndani ya siku kadhaa zijazo kwaajili ya kuidhinishwa.