1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso yatangaza mpango mpana wa kupambana na ugaidi

14 Aprili 2023

Utawala wa kijeshi Burkina Faso umetangaza mpango mpana wa kujitwalia mamlaka makubwa ya kukusanya nguvu na rasilimali ili kukabiliana na hujuma za makundi ya itikadi kali zinaoitikisa nchi hiyo tangu kuanza kwa 2023

https://p.dw.com/p/4Q3qB
Symbolbild Islamisten in Burkina Faso
Picha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/GettyImages

Tangazo lilitolewa na ikulu mjini  Ouagadougou limesema mkakati huo unajumuisha kutangzwa hali ya hatari kwenye maeneo yanayokumbwa na wimbi la mashambulizi ya makundi ya itikadi kali.

Soma pia: Burkina Faso yaishutumu France 24 'kuwasaidia magaidi'

Vile vile utawala wa kijeshi unapanga kuweka utaratibu wa kisheria wa kuwashughulkia wanamgambo watakaokamatwa. Waziri wa Ulinzi wa Burkina Faso  Kassoum Coulibaly kila la raia wa nchi hiyo atakuwa na wajibu wa kushiriki katika kurejesha usalama wa taifa.

Soma pia: Magaidi kadhaa wauawa Burkina Faso

Kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo Ibrahim Traore ambaye alitwaa madaraka kwa mapinduzi Septemba mwaka uliopita, ameweka lengo la kurejesha udhibiti wa asilimia 40 ya ardhi ya Burkina Faso ambayo sasa inakaliwa na wanamgambo wa itikadi kali.